ASILI YA UONGOFUUTHMAN M.ALISKH SAID MOOSADOWNLOADSMIJADALA YA MWEZIISLAMIC TIDES FORUM QUR'AN TAKATIFUISLAMICTIDES

www.asili.islamictides.com

JIVUNIENI UISLAMU WENU
  Vijana wa kiislamu wametakiwa kujivunia uislamu wao kwani utamaduni wa kiislamu kwa sasa ndio unaotawala katika dunia. Mwito huo ulitolewa na sheikh Mohammed Said Albusaidy kwenye hafla fupi ya kuwaaga wanafunzi waliomaliza darasa la saba katika shule ya msingi ya kiislamu ya Jaabir bin Zaid iliyopo barabara ya saba katikati ya jiji la Tanga. Akiwa ndiye mgeni rasmi katika hafla hiyo,sheikh Mohammed alisema hali hiyo ya kuja juu utamaduni wa kiislamu imeibuka kutokana na kushindwa kwa tamaduni nyingine kwenye nchi za kimagharibi hivyo watu kutokuona pahala pengine pa kukimbilia isipokuwa katika uislamu. “Wazungu wamekuwa wakitenda mambo ambayo hata wanyama hawafanyi mbele ya binadamu”,alisema sheikh Mohammed kuwazindua vijana hao.Hali hiyo aliongeza kuwa imewaletea matatizo wao wenyewe,kuwafanya wengi wakimbilie kwenye utamaduni wa kiislamu. Aliwaasa wahitimu hao kuwa waangalifu katika hatua ya masomo yao yanayowakabili kwani huko waendako watakumbana na vishawishi vingi.Aliwaambia hatua hiyo ndiyo itakayowaonesha katika jamii na kujulisha umadhubuti wa msingi waliojengewa shuleni hapo.Aliwataka waangalie mfano katika jengo la kawaida ambapo msingi daima hufichwa na jengo linalofuatia juu yake,lakini umadhubuti wa msingi huonekana kwa namna ambavyo ama jengo hilo litakuwa likifanya nyufa kadiri ujenzi unavyoendelea au kuhimili uzito juu yake bila kuonesha athari hiyo. Wanafunzi hao walitakiwa kuchagua vyema shule za kujiunga kwa ajili ya kuanza elimu yao ya sekondari miongoni mwa shule za kiislamu kwa vile ujenzi wa shule ya sekondari unaoondelea eneo la Machui kwa ajili yao haitoweza kuanza mwaka 2011 kama ilivyokuwa imepangwa awali. Hii ni mara ya mwanzo kwa shule ya Jabir bin Zaid inayomilikiwa na jumuiya ya Ibadhy kutoa wahitimu wa darasa la saba

MWAKA MPYA 1433H
  Kutoka Mimbarini:Na Kaima Mwanjia. ‘’Hakika Ujumbe huu unatokana na Mtume Suleiman,na unaanza kwa:BISMILLAHIR RAHMAA NIR RAHIIM..’’ MWAKA MPYA WA KIISLAM&YATOKANAYO: AlhamduL illaah!tupo ktk Mwaka Mpya wa kiislam, Mwaka[1433-H],Mwaka Mpya ambao Sa haba watukufu wa Mtume[saw]walipendekeza Kalenda ya Kiislam[Mwaka Mpya]uanzie na tukio/tendo la kuhama Mtume[saw]toka Makka kwenda Madina.Kitendo hiki cha kuhama Mtume[saw]toka Makka kwenda Madina kwa lugha ya kisheria hujulikana kama:HIJRAH,ie: Hali ya kuhama waislamu toka sehemu moja kwenda nyingine ili kupata wasaa wa kuabudu ipasavyo/kusimamisha dola ya kiislam! Allah[swt]analithibitisha hilo kwa kusema ‘’Hakika wale watakaofishwa na Malaika hali ya ku wa wamezidhulumu Nafsi zao[wataambiwa na Malaika]Mlikuwa wapi?watasema:[sisi]tuliku wa wanyonge kule duniani,hivi/kwani haikuwa ardhi ya Allah[swt]ni yenye wasaa[NafasiMka hamia huko?hao[sote tutakaokufa kabla ya Dola ya Kiislam kusimama]Makazi yao ni Jahann am,nay awe ni Marejeo mabaya kabisa’’ [4:97] Sababu ya kimsingi kabisa iliyopelekea Mtume[saw]ahame toka Makka kwenda Madina ni Ukosefu wa Uhuru wa Kuabudu[Lacking of FREEDOM Worsship],hali iliyomsibu Mtume[saw] ktk kipindi chote alichokuwepo Makka,na ndio hali inayotusibu sisi Waislamu wa leo kwa kiw ango cha kutisha!Hatuwezi kudai/kusema kuwa tunao Uhuru wa kuabudu ndani ya Nchi yetu hii il-hali hatuna Mamlaka ya kutekeleza amri ya Allah ya Kukata Mwizi Mkono kupitia Jinai hi Pia tutakua hatuna haki ya kudai kuwa tunao Uhuru wa Kuabudu,hali ya kuwa hatuna Mamla ka ya kuwapiga kwa Mawe hadi kufa[Wazinzi waliokwisha Owa/Kuolewa]na hatuwachapi Vi book[Wazinzi ambao hawajaowa/kuolewa]. Si hivyu tu,bali pia hatuna haki ya kudai kuwa tunao Uhuru wa Kuabududu,hali ya kuwa Jamii yetu imejaa Walevi wanaotuchafulia Mazingira kwa Matusi na kukojoa hovyo Barabarani na tukawa hatuna Mamlaka ya kumchapa VIBOKO[80]Mkosaji huyu,kama inavyoagiza Sheria ya Uislamu. Hatuna haki pia ya kudai kuwa tunao Uhuru wa kuabudu,il-hali ndani ya Jamii tunayoishi tu nalazimishwa kuwatambua Watoto wa Nje ya Ndoa kuwa ni Watoto halali,Wanastahiki kuri thin a kupata haki zote kama ilivyo kwa Watoto wengine. Kama yote hayo hayatoshi kuwa hoja,lakini pia hatuna haki ya kudai kuwa tunao Uhuru wa kuabudu,il-hali ndani ya Jamii yetu tunayoishi Mikataba miwili[2]ya ajabu,inayofedhehesha, kusikitisha&kuhuzunisha,Mikataba inayoruhusu Ndoa za jinsia moja,yani Mwanamme kwa Mwanamme&Mwanamke kwa Mwanamke!!! Si hivyo tu,bali Mikataba miwili hii,pamoja na mambo mengine inayo Mamlaka,Nguvu na uw ezo wa kuwaenzi na kuwalinda ‘’WAOVU WA MATENDO’’ hawa wasibughudhiwe. Mikataba hii ni maarufu kwa Majina ya:TRIPR[Trade Related Interllectual Propert Right] na TRIM[Trade Related Investment Measure]Na kwa hivi sasa tayari Mikataba miwili hii ina bara Ka zote toka Uingereza&Marekani. Kwa kuwa Mtume[saw]alihama toka Makka kwenda Madina,hali iliyopelekea kuwa na Kalen nda ya Kiislam,tunajifunza kuwa kuhama toka sehemu moja hadi nyingine kwa ajili ya Ukosef wa Uhuru wa kuabudu ni Ibada km zilivyo Ibada nyingine.Isipokuwa Ibada hii ya kuhama Mtu me[saw]aliisitisha mara baada ya ‘’FAT-HU MAKKA’’[Kukombolewa Makka],Mwaka wa 8 wa Hijra. Katika hadithi iliyopokewa na Swahaba mtukufu Ibn Abbas na kuthibitishwa hadithi hiyo na Imam Bukhari,Mtume[saw]anaasema:’’Hapana Hijra[kuhama]baada ya kukombolewa Makka [ila kilichopo]ni Juhudi ya dhati na Nia madhubuti’’ Anachotaka tukifahamu Mtume[saw]kupitia hadithi hii ni Kutoyakimbia Mazingira yetu maba ya tunayoishi nayo ktk Jamii,bali tubaki ktk Mazingira hayo huku tukiwa na Mikakati na Juhu di za makusudi ktk kuubadilisha uozo na uchafu uliomo ndani ya jamii zetu,na si kuikimbia Jamii kwa kuchelea yasije yakatufika na kutupata km yaliyompata Mtume Yunus[a.s]. Kuhama kwa Mtume[saw] kunatupa Mafunzo&Mazingatio makubwa ktk maisha yetu ya kila siku,Miongoni mwa Mafunzo hayo ni pamoja na Haja,ulazima na umuhimu wa kuyaendesha mambo yetu mbali mbali ya kijamii na kibinafsi ktk hali ya kushaurizana[mutual consultation] Msikiti kuwa ndio chimbuko na kitovu cha harakati za kiislamu.Lakini pia kwa safari ya Mtum [saw]ya kuhama toka Makka kwenda Madina,tunajifunza kuwa Mtume[saw]alikuwa Kiongozi na si Mtawala,kwa maana alikuwa akijituma ktk kufanya kazi pamoja na majukumu yake ya kiuongozi.Na hilo linadhihirika kwa namna Mtume[saw]alivyoshiriki kimwili ktk ujenzi wa Msi kiti ulioitwa kwa jina lake[Masjidun-Nabawiy].Mwanachuoni Swafiyyur-Rahmaan ktk kitabu chake Arrahiiqum-Makh’toum,ukurasa 184 ‘’Mtume[saw]kwa mkono wake mtukufu alibeba Mawe,Matofali il-hali anasema ‘’Ee!Mungu hakuna maisha ila maisha ni ya akhera,wasameh Ansaar&Muhaajir’’.Huu ulikuwa ndio wasifu wa Mtume[saw]km Kiongozi wa kijamii,kwa ma ana hakubweteka kukaa ofisini hata siku moja na kuagiza watu wa chini yake wafanye kazi kwa niaba yake!Mtunzi wa kitabu cha orodha ya watu Mia moja[100]mashuhuri duniani[Mic hael.H.Hatt]analithibitisha hilo kwa kusema ‘’He was the only man in history,who was suppr emely successfull on both,religious and secular level’’,akimaanisha kuwa Mtume Muhamad ni kiongozi pekee ktk jamii ya Mwanadamu aliefanikiwa kwa kiwango cha juu ktk Uongozi wa ke. Wabillahit-Tawfiiq|ASILI YA UONGOFU| |UTHMAN M.ALI| |SKH SAID MOOSA| |DOWNLOADS| |MIJADALA YA MWEZI| |ISLAMIC TIDES FORUM| | QUR'AN TAKATIFU| |ISLAMICTIDES|