ASILI YA UONGOFUUTHMAN M.ALISKH SAID MOOSADOWNLOADSMIJADALA YA MWEZIISLAMIC TIDES FORUM QUR'AN TAKATIFUISLAMICTIDES

MIJADALA YA MWEZI NA KALENDA


بسم الله الرحمن الرحيم Ili kufanikiwa kumimina mjadala unaotaka chagua na halafu right click uchague unachopendelea.

KUSOMEA CHINI YA MTI

     Wasomaji wa kisa hiki naomba tukubaliane kuwa mfumo wa elimu yetu, Tanzania bado umejikita katika kupima uwezo wa wanafunzi kukariri majawabu vizuri na kufaulu mitihani. Kwa sisi ambao tulisomea A-level kwenye shule zilizoanzishwa kwa haraka za malengo ya kisiasa tuliathirika sana Download KUSOMEA CHINI YA MTI MUM.pdf

MJADALA WA MWEZI EACROTANAL ZANZIBAR MWAKA 1991

     Mjadala wa mwezi ulikuwa ni sehemu ya kongamano lililotolewa anuani ya “Semina ya Kiislamu Zanzibar”. Mada nyengine zilizojadiliwa kwenye semina hiyo ni Sala ya Ijumaa na Adhuhuri, Makaburi, Khitma na mambo anayofanyiwa maiti, Maulid na talaka tatu. Sisi tutachukua mjadala wa mwezi tu, uliochukua nafasi zaidi. Semina ilifunguliwa na aliyekuwa rais wa Zanziabar bwana Salmin Amour Juma na yeye ndiye aliyeifunga. Masheikh maarufu waliohudhuria semina hiyo ukiondoa watoa mada ni pamoja na marehemu Skh Ameir Tajo, Skh Ameir Tajo mdogo, Skh Nurdeen Hussein Shaadhily. Hawa ni wachache tu niliowataja kutoka ukumbi uliojaa. Download KONGAMANO LA MWEZI-EACROTARNAL.pdf

MJADALA WA MWEZI KENGEJA 1995

     Ndugu waislamu. Kwa niaba ya mkuu wa wilaya, nimesimama hapa kuzungumza machache kuhusiana na mkusanyiko wetu huu. Kwa bahati mbaya mkuu wa wilaya mwenyewe amedharurika na huu ujumbe itabidi uwafike, kwa niaba yake nimesimama hapa kuufikisha ujumbe huo. Download MJADALA+WA+MWEZI+KENGEJA.pdf

MUHTASARI KONGAMANO LA KIBAHA-1998

     Kongamano lilipoanza wajumbe walikuwa wamejipanga kwenye meza mbili ndefu ambazo wajumbe wakikaa wanaangaliana.Upande mmoja wakakaa wajumbe wa upande wa Bakwata na upande mwengine wajumbe wa upande wa Ansaar Sunna.Sehemu ya meza kuu katikati ya ncha mbili za meza hizo walikaa sheikh mkuu,marehemu sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed na naibu mufti wa Zanzibar. Download MUHTASARI WA KONGAMANO LA MWEZI.pdf

INTERNATIONAL SYMPOSIUMS ON MOONSIGHTINGS

Download INTERNATIONAL  SYMPOSIUMS  ON MOONSIGHTING  AND SCIENCE  OF       THE  MOON.pdf

MASHEIKH TWENDE MWEZINI

     Mwezi, huu unaoipa nuru dunia katika baadhi ya siku ni sayari (satellite) pekee inayoizunguka dunia katika hali ya kimaumbile. Mwezi hauna nuru yake wenyewe bali ni muangaza wa jua unaotua juu yake ndio unaoufanya ung'are. Ni moja ya kumi tu (1/10) ya muangaza inaopokea kutoka kwenye jua ndio unaouakisi (reflect) na kuleta mng'aro kwa dunia. Download MASHEKHE TWENDE MWEZINI.pdf

KUPWA NA KUJAA KWA BAHARI

     Kupwa na kujaa kwa bahari daima huwa kunapishana kwa wastani wa masaa 6.Katika kipindi hicho pwani zinakuwa na moja kati ya matukio mawili hayo;ama kujaa kwa bahari au kupwa kwa bahari. Download KUPWA NA KUJAA KWA BAHARI.pdf

MAWIMBI KAMA KIOO CHA KUUANGALIA MWEZI

     Bahari katika dunia ni asilimia 71 ya eneo lote la dunia.Hii 71% ya eneo la dunia ni sawa na 361 million square kilometres au 140 million square miles.Wastani wa kina chake kwenda chini ni 5000m au 16000ft.Kwa takwimu hizi,ina maana kuwa asilimia kubwa ya wakazi wa dunia wako karibu ya bahari na wanategemea bahari kwa maisha yao. Download MAWIMBI  KAMA KIOO CHA KUUANGALIA MWEZI.pdf

NAMNA YA KUTENGENEZA KALENDA YA KIISLAMU YA MAWIMBI YA BAHARI

     Ili kupata kalenda ya mfano ya kiislamu ya mawimbi ya bahari,tutatumia kalenda nne tofauti za kiislamu kama zilivyochapishwa mwaka 2006.Mbili kati ya hizo kwa mtazamo wangu zina msimamo wa mwezi wa kimataifa na mbili ni za msimamo wa kila nchi na mwezi wao.Kalenda tunayotarajia kuitayarisha itakuwa ni tofauti na kalenda zote hizo tulizozitaja. Download KUTENGENEZA KALENDA YA KIISLAMU YA MAWIMBI YA BAHARI.pdf

DHUL HIJJA 1433H.

     Sample islamic-tides calendar for Dhulhijja 1433. Download ISLAMIC KALENDA-dhulhija 1433.doc|ASILI YA UONGOFU| |UTHMAN M.ALI| |SKH SAID MOOSA| |DOWNLOADS| |MIJADALA YA MWEZI| |ISLAMIC TIDES FORUM| | QUR'AN TAKATIFU| |ISLAMICTIDES|